c. semi za Paulo (Rum. 11:22; 1 Kor. 15:2; 2 Kor. 13:5; Gal. 1:6; 3:4; 5:4; 6:9; Flp. 2:12; 3:18-20; Kol.
1:23; 2 Tim. 3:2)
d. semi za mwandishi wa Kiebrania (2:1; 3:6,14; 4:14; 6:11)
e. semi za Yohana (1 Yohana 2:6; 2 Yohana 9; Ufu. 2:7,17,26; 3:5,12,21; 21:7)
Mambo ya wokovu ndani ya biblia hutoka katika pendo, huruma, na neema ya mamlaka ya Mungu wa Utatu.
Hakuna mwanadamu awezaye kuokolewa pasipo kuingiliwa na Roho (kama vile Yohana 6:44,65). Mungu
alikuja na kupangilia mambo muhimu, lakini alidai kwamba wanadamu wanapaswa kuitikia katika imani na
toba, katika namna zote kwa uanzilishi na kwa uendelevu. Mungu hutenda kazi na wanadamu katika
uhusiano wa agano. Kuna upendeleo na majukumu!
Wokovu umetolewa kwa wanadamu wote. Kifo cha Yesu kilihusika na tatizo la dhambi ya uumbaji
ulioanguka! Mungu ameleta njia na anahitaji wale wote walioumbwa kwa mfano Wake kuliitikia pendo Lake
na utoaji katika Yesu. Kama ungependa kusoma zaidi juu ya somo hili tazama
1. Dale Moody, The Word of Truth, Eerdmans, 1981 (kur. 348-365)
2. Howard Marshall, Kept by the Power of God, Bethany Fellowship, 1969
3. Robert Shank, Life in the Son, Westcott, 1961
Biblia inashughulikia matatizo mawili tofauti katika eneo hili: (1) kuchukulia imani kama msimamo wa kuishi
bila kuzaa matunda, maisha ya ubinafsi au (2) kuwatia moyo wale wanaopambana na huduma na dhambi
binafsi. Tatizo ni kwamba makundi yasiyo sahihi yana uchukuwa ujumbe usio sahihi na kutengeneza mifumo
ya kitheolojia yenye vifungu vya kibiblia vyenye kuwekewa mipaka. Baadhi ya Wakristo wakiwa katika hali ya
kukata tamaa wanahitaji ujumbe wa kuwatia moyo, wakati wengine wanahitaji kuonywa kwa ukali kuhusiana
na uvumilivu! Wewe uko ndani ya kundi lipi?
Kuna mabishano ya historia ya kitheolojia iliyomuhusisha Augustine dhidi ya Pelagius na Calvin dhidi ya
Arminius (semi-Pelagian). Jambo hili lilihusisha swali la wokovu : kama mtu akiokolewa kiukweli, yampasa
kustahimili katika imani na uamiifu?
Wafuasi wa Calvin wamesimama nyuma ya maandiko yale ya kibiblia ambayo yanadai kwamba mamlaka ya
Mungu na nguvu idumuyo (Yohana 10:27-30; Rum. 8:31-39; 1 Yohana 5:13,18; 1 Pet. 1:3-5) na vitenzi vya
nyakati kama kauli tendewa timilifu endelevu ya Efe. 2:5,8.
Wafuasi wa Arminius wamesimamia maandiko yale ya kibiblia ambayo yanamuonya yule aaminiye "kusimama
imara," "kudumu," au "kuendelea" (Mt. 10:22; 24:9-13; Marko 13:13; Yohana 15:4-6; 1 Kor. 15:2; Gal. 6:9;
Ufu. 2:7,11,17,26; 3:5,12,21; 21:7). Mimi binafsi siamini kwamba Waebrania 6 na 10 zinatumika, lakini
wafuasi wengi wa Arminius wanazitumia kama onyo dhidi ya uasi. Mfano wa Mpanzi katika Mathayo 13 na
Marko 4 inashughulikia suala la imani, kama inavyofanya Yohana 8:31-59. Kama wafuasi wa Calvin wanavyo
nukuu vitenzi vya kauli ya wakati uliopo timilifu vilivyotumika kueleza wokovu, Wafuasi wa Arminius wana
nukuu vifungu vya kauli ya wakati uliopo kama 1 Kor. 1:18; 15:2; 2 Kor. 2:15.
Huu ni mfano kamili wa namna mfumo wa kitheolijia unayotumiwa vibaya njia ya uhakiki wa fasiri za
maandiko. Mara nyingi kanuni inayoongoza au andiko kuu linatumika kutengeneza ufito wa
kitheolojia ambapo maandiko mengine yote yanatazamiwa. Kuwa makini na mfumo kutoka vyanzo
vyo vyote vile. Vitokana na ufafanuzi wa mantiki ya mashariki, si ufunuo. Biblia ni kitabu cha
mashariki. Inawakilisha kweli katika mvutano uliokamilishwa, ulinganifu wa mafumbo
yaonekanayo. Wakristo wanamaanisha kukubaliana na yote na kuishi ndani ya mvutano huo. Agano
Jipya linawasilisha vyote yaani ulinzi wa mwaamini na dai la imani endelevu na uovu. Ukristo ni
mwitikio wa mwanzo wa toba na imani inayofatiwa na mwitikio endelevu wa toba na imani. Wokovu
si kama matokeo (tiketia ya kwenda mbinguni au sera ya bima ya moto), bali uhusiano. Ni maamuzi
na uwanafunzi. Inaelezwa katika Agano Jipya 3:5
utimilifu (tendo lililokamilishwa na matokeo endelevu), Efe. 2:5,8
inawasilisha (tendo endelevu), 1 Kor. 1:18; 15:2; 2 Kor. 2:15
wakati ujao (matukio yajayo au matukio fulani), Rum. 5:8,10; 10:9; 1 Kor. 3:15; Flp. 1:28; 1 The. 5:8-9;
Ebr. 1:14; 9:28
katika vitenzi vyote vya nyakati:
kauli (tendo timilifu), Matendo 15:11; Rum. 8:24; 2 Tim. 1:9; Tito